WAZIRI NAPE, AVIFUNGUIA VITUO VYA RADIO 5 NA MAGIC FM KWA MADAI YA UCHOCHEZI

Image result for radio banned images


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam kwa sababu za uchochezi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Waziri Nape amesema kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti  vilitangaza habari ambazo ndani yake zina uchochezi.

“Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo (Agosti 29 2016) hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake,” alisema Nape.

Aidha, amesema kuwa ameiagiza Kamati ya Maudhui ya vyombo vya habari kuviita vyombo hivyo na kuvihoji kwa kina kisha kumshauri hatua zaidi ya kuchukua.

Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kutambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari katika kuleta amani na ushirikiano nchini na sio vinginevyo.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.