ALICHOSEMA RIDHIWANI KIKWETE BAADA YA KUONEKANA KWENYE PICHA MOJA NA LOWASSA



Jumapili hii Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete(CCM), amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake hususan waliomtangulia.
Ridhiwani ametumia Instagram kuelezea hilo baada ya kukutana na aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.
“Siasa ni shule ambayo haina mwisho. nahisi bado niko shule ya msingi na ninaendelea kujifunza,” ameandika.
Mbunge huyo alimfuata Lowassa alipokuwa amekaa na kufanya naye mazungumzo ambayo hajayaweka wazi, na kisha kurudi sehemu yake huku akishuhudia timu yake ya Yanga iliyofungwa 2 – 1 na Simba.
Wengi wamefurahishwa na maneno hayo huku wakimpongeza mbunge huyo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.