TIOB YAZINDUA RASMI DODOSO LA MAPITIO YA WANACHAMA WAKE +PICHA
Tanzania Institute of Bankers (TIOB) imezindua rasmi
mfumo/Dodoso kwa ajiri ya kukusanya maoni na mapendezo ya wanachama juu ya
ufanisi wa kozi na mitihani ya taaluma ya kibenki zinazotolewa pamoja na maoni
ya watanzania kwa ujumla watakaopenda kujua zaidi kuhusu TIOB kupitia barua
pepe na tovuti ya taasisi.
TIOB ni taasisi inayosimamia taaluma ya sekta ya
kibenki Tanzania ambayo inashirikiana na mabenki yote yaliyopewa leseni na
benki kuu, inafanya usiamamizi huu kwa kutoa vyeti vya taaluma kwa wanachama
pamoja na kutunza taarifa zao.
Leo tunatangaza rasmi kwanzia tarehe 31 Jully 2017
mpaka 30 September 2017 tutakua tunapokea maoni ya wanachama na watanzania wote
mabao wangependa kujua juu ya kozi na huduma nyingine zinazotolewa na TIOB kupitia
tovuti ya taasisi ambayo ni www.tiob.or.tz
Aidha, TIOB imetangaza matokeo ya mwezi May 2017, Ndugu
Saad Banzi – Msajili wa TIOB ameyatangaza
matokeo hayo ya watahiniwa katika mithani ya Nyanja ya kibenki, ambapo kulikua
na watahiniwa 800 walijisajili kwa ajili ya mitihani, katika hao watahiniwa 115
waliweza kufaulu mitihani yao katika Nyanja za Certificate of Banking (9), Certified
Proffesional Bnkers ( 97) na Specialist Programs (9).
Idadi hii ya watahiniwa 800 waliojisajili ni kati ya
wafanyakazi wa sekta ya benki 15,000 walioko nchini, vile vile taasisi imeanza
kupokea maombi kwa wale wanaohitaji kufanya mitihani hiyo kwa mwezi wa November,
wanaweza kufika ofisi za taasisi zilizoko Mirambo Street/Samora NIC House 10th
floor.
Mkurugenzi wa mafunzo ameongeza kwa kutaja kozi za
muda mfupi zinazotolewa na taasisi ambapo kwa mwezi wa nane, kutakua na kozi za
:
Ø Assets
and liability Management ( 9 – 11 Aug 2017 )
Ø Bank
Branch Management ( 15 – 18 Aug 2017)
Ø Sales
and Customer Care ( 22 – 25 Aug 2017 )
“TIOB imejipanga kuendana na uvumbuzi ambao umefika
hapa nchini, wa aina ya huduma za kibenki na ule wa kidigitali katika hutoaji
wa huduma za sekta hii ya kibenki ambao kwa kiasi kukibwa umesaaidia nchi kukua,
taasisi hii inatoa elimu na kuwaanda wahitimu wake kwa kufuata misingi ya sharia
ya utoaji huduma katika sekta ya kibenki,” – Patrick Mususa Mkurugenzi Mtendaji
wa TIOB
Kwa taarifa hizi, Taasisi inaomba ushirikiano katika
kujaza na kujibu maswali mbalimbali yaliyopo kwenye dodoso hilo, kwa usahihi na
ukweli kwaajili ya kufanikisha mapitio haya.
Kwa Taarifa
Zaidi wasiliana na:
The Executive
Director
Tanzania
Institute of Bankers
P. o. Box 8182, Dar
es Salaam.
Telephone: 22
2112605
Email:
info@tiob.or.tz
No comments:
Post a Comment