UCHAGUZI MAREKANI, DONALD ,HILLARY WASHINDA NEW YORK , + UTARATIBU WA UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI

NEWS UPDATES.
Donald na Hillary washinda New York: URAIS MAREKANI 2016,( DONALD VS HILLARY CLINTON.)

Zaidi ya nusu ya kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani katika mji wa New york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton wamepata ushindi mkubwa Zaidi ndani ya vyama vyote viwili.
Hillary Clinton ambaye amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa ameeleza katika hotuba yake kuwa ushindi wa chama chake cha Democratic umeweza kuwaunganisha zaidi wapinzani wake kuwa wamoja Zaidi ya kuwagawa.
Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Repubilcan .
Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa .Hillary amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja Zaidi ya kuwagawa.

Utaratibu wa kuchagua wagombea Marekani uko hivi.... 


Wanasiasa wanaotaka kuwania urais Marekani kupitia vyama mbalimbali wamekuwa wakikabiliana kwa miezi kadha sasa vyamani, lakini umefika wakati wa wananchi kuamua nani atapeperusha bendera.
Lakini je, ni utaratibu gani hufuatwa?
Mkutano wa kuwachagua wagombea uliofanyika Iowa ulikuwa wa kwanza katika msururu wa uchaguzi na mikutano katika majimbo yote ya Marekani.

Mchujo wa kuteua wagombea na umuhimu wake

Mshindi wa kila uchaguzi hupata wajumbe kadha, - wanachama wa chama ambao hukutana Julai kuidhinisha wagombea.
Mgombea anavyoshinda katika majimbo mengi, ndivyo anavyopata wajumbe wengi wa kumuunga mkono mkutano wa mwisho wa kuidhinisha wagombea.
Kwa kuwa Rais Barack Obama hawezi kuwania tena, vyama vyote viwili vinaanda uchaguzi kamilifu.
Mgombea wa Republican atahitaji wajumbe 1,237 ili kushinda, naye mgombea wa Democratic atahitajika kupata wajumbe 2,383.

Tofauti ni gani baina ya uchaguzi wa kuteua wagombea na mkutano wa kuteua wagombea

Kuna njia kadha tofauti za kuchagua wajumbe kupitia uchaguzi wa awali (primaries).
Uchaguzi ulio wazi hushirikisha wapiga kura wote waliojiandikisha katika jimbo husika, na wanaweza kupigia kura mgombea yeyote. Mpiga kura wa Republican anaweza kushiriki uchaguzi wa kuteua mgombea wa Democratic kwa mfano.
Katika uchaguzi usio wazi, ni wapiga kura wanachama wa chama pekee wanaoruhusiwa kushiriki.
Aidha, kuna uchaguzi mseto, ambapo wapiga kura wa chama pinzani hawaruhusiwi kushiriki lakini wapiga kura huru wanaruhusiwa kushiriki.
Mikutano ya kuteua wagombea (caucuses) ni mikutano ambayo huhusisha wapiga kura kuonyesha uungaji mkono wao kwa wagombea kwa kuinua mikono. Kawaida, ni wapiga kura waliosajiliwa pekee, ambao ni wafuasi wa chama husika cha siasa, hushiriki.





TrumpImage copyrightAFP
Image captionDonald Trump anaongoza kwenye kura za maoni chama cha Republican

Hufanyika lini na wapi?

Uchaguzi wa awali wa kuteua wagombea huendelea hadi Juni, lakini uchaguzi wa mapema ndio husisimua sana kwani huashiria mwelekeo wa kinyang’anyiro.
Mbio hizi hufikia kilele kawaida tarehe 1 Machi au ‘Jumanne Kuu’ ambapo karibu majimbo 13 hufanya uchaguzi au mikutano ya kuteua wagombea siku moja.
Vyama vyote viwili huandaa uchaguzi wa awali au mikutano ya kuchagua wagombea siku moja, mara nyingi.

Februari:

Wagombea kujaribu kujijengea msingi na kusalia kwenye kinyang’anyiro.
1 Feb: Mikutano ya Iowa
9 Feb: Uchaguzi wa New Hampshire
20 Feb: Mikutano ya Nevada (Democratic), Uchaguzi wa South Carolina (Republican)
23 Feb: Mikutano ya Nevada (Republican)
27 Feb: Uchaguzi wa South Carolina (Democratic)

Machi:

Majimbo 13 hupiga kura Jumanne kuu ikiwa ni pamoja na majimbo sita Kusini. Ni nafasi nzuri kwa mgombea kujithibitishia ubabe, ingawa bado mambo huwa yanaweza kubadilika baadaye.
1 Machi – ‘Jumanne Kuu': Mikutano ya Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia Primaries; Alaska & Wyoming (Republican), Colorado Caucuses (Democratic)
5 Machi: Mikutano ya Kansas, Uchaguzi Louisiana, Mikutano Kentucky & Maine (Republican), Mikutano Nebraska (Democratic)
6 Machi: Mikutano ya Maine (Democratic)
8 Machi: Mikutano ya Hawaii & Idaho (Republican), Uchaguzi wa Idaho (Republican), Michigan & Mississippi
15 Machi: Uchaguzi wa Florida, Illinois, Missouri, North Carolina, Ohio
Kuna majimbo makubwa ambayo yatakuwa yakipigania mwezi Machi, hasa majimbo ambayo mshindi hupokea wajumbe wote. Pia kuna majimbo yasiyo na msimamo mkali ambako kuna uwezekano mkubwa kwa wagombea kuwashawishi wapiga kura kubadili msimamo.
22 Machi: Uchaguzi Arizona, Mikutano Utah, Mikutano Idaho (Democratic)
26 Machi: Mikutano ya Alaska, Hawaii, Washington Caucuses (Democratic)

Aprili-Mei






ClintonImage copyrightAP
Image captionHillary Clinton anaongoza kwenye kura za maoni chama cha Democratic

Uchaguzi katika majimbo haya huenda ukawa muhimu zaidi kuliko kawaida kwa chama cha Republican kutokana na na kuwepo kwa wagombea waliofadhiliwa vyema mwaka huu, ambao wanaweza kusalia mbioni hadi Aprili.
1 Aprili: Mikutano North Dakota (Republican)
5 Aprili: Uchaguzi Wisconsin
9 Aprili: Mikutano ya Wyoming (Democratic)
19 Aprili: Uchaguzi wa New York
26 Aprili: Uchaguzi wa Connecticut, Delaware, Maryland, Pennsylvania, Rhode Island
3 Mei: Uchaguzi wa Indiana
10 Mei: Uchaguzi wa West Virginia, Uchaguzi wa Nebraska (Republican)
17 Mei: Uchaguzi Oregon, Uchaguzi Kentucky (Democratic)
24 Mei: Uchaguzi wa Washington (Republican)

Juni

7 Juni: Uchaguzi California, Montana, New Jersey, New Mexico, South Dakota; North Mikutano Dakota (Democratic)
14 Juni: Uchaguzi wa District of Columbia (Democratic)
18-21 Julai: Kongamano Kuu la Kitaifa la Wajumbe wa Chama cha Republican
25-28 Julai: Kongamano Kuu la Kitaifa la Wajumbe wa Chama cha Democratic

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.