PIPI ZENYE SUMU ZAUA WATU 23 PAKISTAN

Pipi hizo hujulikana kama ladoo.
Polisi nchini Pakistan wanasema kuwa huenda watu 23 waliofariki mwezi jana baada ya kumumunya peremende, huenda waliaga dunia kutokana na sumu iliyotiwa ndani ya peremende hizo na nduguye mwenye duka.

Inaarifiwa kuwa kijana huyo Khalid Mahmood, amekiri kuchanganya peremende hizo na dawa ya kuangamiza wadudu, katika kitendo cha kulipiza kisasi baada ya majibizano kati yao.

Kilikuwa kisa cha kushangaza.

Kwa kawaida watu hununua pipi hizo, kwa jina Ladoo kwa wingi na kuwagawia marafiki na jamaa wakati wa sherehe.

Nduguye mwenye duka anasema alitia sumu kwenye pipi baada ya ugomvi.


Mwanamme mmoja alinunua pipi hizo na kuwapa watu wakati wa sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa mwanawe wa kiume.

Yeye pamoja na jamaa wake 11 waliaga dunia.

Hatua ya Mahmood kukiri kutekeleza uhalifu huo inaongeza suitafahamu kuhusu nini hasa kilitokea kwani taarifa zinasema watu wengine wawili wamekiri kuhusika katika mauaji hayo.



No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.