TIMU MBILI TU ZA UINGEREZA NDO ZIMEWAHI KUONDOKA BERNABEU NA USHINDI, MAN CITY ITAKUA YA TATU?





4 May 2016
By Shafffi Dauda

Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya pili ya Champions League kati ya Los Blancos vs Manchester City,  rekodi ya Real Madrid ya nyumbani katika mechi za ulaya dhidi ya vilabu vya England ni nzuri sana. 

 Kati ya mechi 14 walizocheza dhidi ya vilabu vya Malkia wa Uingereza katika dimba la Santiago Bernabeu, Los Blancos wameshinda mechi 7, sare 5 na wamepoteza mbili – katika hatua ya raundi ya 16 bora. 



Mechi ya kwanza kupoteza ilikuwa dhidi ya kikosi cha Arsene Wenger mwaka 2006 – goli la kipindi cha pili la Thierry Henry lilitosha kuiondoa Madrid katika michuano. 

Mechi iliyofuata ilikuja baada ya miaka 3 dhidi ya kikosi cha Liverpool cha Rafael Benitez – goli la kichwa la Yossi Benayoun kiliwapa nafasi majogoo wa jiji kuelekea mchezo wa marudianopale Anfield. Mechi ya pili Madrid wakafungwa tena huku mechi zote zikiwa na marefa wa kiitalia.



 Tangu wakati huo Madrid wamekuwa na rekodi nzuri wakishinda mechi 3 kati ya 4 za nyumbani dhidi ya vilabu Vya England-  Tottenham (2011), Manchester City (2012) na Liverpool (2014);

 Ushindi wao maarufu zaidi ulikuja dhidi  Derby County katika kombe la ulaya hatua ya mtoano mwaka 1975; Charlie George alifunga hat trick wakati Derby waliposhinda 4-1 katika uwanja wao wa Baseball Ground. Mchezo wa pili Madrid wakabadili matokeo kupitia magoli ya Santillana. 

Lakini usiku wa leo Los Blancos wanahitaji kushinda tu na sio sare – matokeo ambayo yametokea mara 5 dhidi ya vilabu vya England. Waliwahi kutolewa kwenye UEFA Cup na kikosi cha Ipswich cha Bobby Robson mnamo mwaka 1973 baada ya mechi ya marudiano pale Santiago Bernabeu kuisha kwa sare huku mechi ya kwanza ikiisha kwa ushindi wa 1-0 kwa waingereza. 




 Manchester United wamefanikiwa kutoka Bernabeu na sare mara mbili – mwaka 1968 mechi iliisha kwa sare ya 3-3 kwenye nusu fainali, na sare ya 1-1 wakati Cristiano aliposawazisha goli la Danny Welbeck mnamo February 2013 katika hatua ya mtoano. 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.