UEFA YAWAPIGA ADHABU MASHABIKI WA RUSSIA KWENYE EURO 2016
Russia wataondolewa katika michuano ya Euro mwaka huu ikiwa tu watathibitika kufanya vurugu tena kufanya vurugu katika michezo iliyobaki.
Kwa mujibu wa ‘European football’s governing body’, Russia wamepewa onyo na pamoja na adhabu ya kupigwa fainai ya Euro 150,000 (sawa na paundi 19,000) kutokana na vurugu zilizojitokeza katika mchezo dhidi ya England uliofanyika Marseille.
Russia pia wameshtakiwa kwa kashfa ya ubaguzi wa rangi na kujihusisha na uwashaji moto wakati wa mchezo.
Adhabu hiyo ya kuondolewa mashindanoni itatekelezwa kwa matukio yote ya uvunjaji sheria yatakayofanyika ndani ya uwanja tu. Milango ya kukata rufaa bado iko wazi.
Hata hivyo, Waziri wa michezo na rais wa Chama cha Soka nchini Russia Vitaly Mutko wamesema kwamba, Russia watatoa malalamiko yao juu ya maamuzi hayo ya UEFA.
Maafisa wa polisi nchini Ufaransa wamesema kwamba, kikosi cha wahuni 150 kilichokuwa na mafunzo maalum kilifanya vurugu kabla ya mchezo wa Russia na England. Mashabiki sita wa England jana walihukumiwa kifungo kwa makosa ya kuvunja sheria.
Zaidi ya watu 35 walijeruhiwa, wengi wao wakiwa ni mashabiki wa England (wanne wakipata majeraha makubwa sana), huku jumla ya watu 20 wakikamatwa baada ya siku tatu kutokana na makosa hayo.
Ikumbukwe tu kwamba mwaka 2012, Russia walinyang’anywa pointi sita na kufungiwa miaka mitatu na nusu baada ya mashabiki wao kuonesha vitendo vya utovu wa nidhamu na adhabu hiyo kuisha baada ya kufuzu michuano ya mwaka huu
No comments:
Post a Comment