FRIDAY XO : ELEWA MIGOGORO KATIKA MAPENZI NA MAMBO YA KUFANYA UFURAHIE MAHUSIANO




Migogoro haiepukiki katika maisha lazima migogoro itokee kwa sababu ya mambo mbalimbali kama vile kitabia, lakini wakati huo huo migogoro kwa namna fulani migogoro fulani husaidia katika:

* Kujitambua
* Kujichuja kujua tabia ya mtu alivyo
* Husaidia kujua msimamo wa mtu mwingine
* Husaidia kuchomoza kwa mtu mwingine

SABABU ZA MSINGI ZA MIGOGORO KATIKA MAPENZI:

>> Maeneo  Tuliyotoka na Tuliyozaliwa.

Utofauti wa maeneo ni chanzo cha migogoro kwa sababu kila jamii au familia huzaliwa katika mitazamo fulani, au uthamani fulani. Hivyo utofauti huo huleta migogoro.

>> Muonekano 

Binadamu hutofautiana, Tumetofautiana katika maeneo makuu manne (katika mawasiliano).

>> Namna tunavyotenda mambo yetu: 

katika kundi hili wapo wanaotenda mambo yao haraka wengine kwa wastani na wengine taratibu, hivyo hata katika mapenzi tofauti hizi hujitokeza.

>> Tofauti katika mapenzi: 

Katika hili hutofautiana kwa kiasi kikubwa kwani wapo wanaopenda kubembelezwa na wale wasiopenda kubembelezwa, wengine wapo kimvuto zaidi na wengine  hapana.

>> Masuala ya uchumi na fedha:

 Watu hutofautiana katika kupata fedha, katika suala zima la matutumizi ya pesa, migogoro mingi katika familia za Tanzania na duniani husababishwa na fedha kwani watu hutofautiana katika kipato.

>> Matarajio:

Jambo lingine linalosababisha migogoro katika maisha ya kimahusiano na ya kikazi katika mapenzi ni matarajio. Watu wengi huwa na matarajio fulani lakini wengi wao wanapoingia na kukuta ndivyo sivyo na
matarajio, huibua migogoro.

>> Kukosa Imani:

Kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu katika maeneo ya kazi na mahusiano huzua migongano: Katika maeneo ya kazi uaminifu unapotoweka ndipo makundi na unafiki huibuka, pia katika mapenzi msipo aminiana lazima kutakuwa na migogoro.

>> Ubinafsi 

Watu wengi wana tabia ya ubinafsi hivyo wanasababisha migogoro katika mahusiano ya kimapenzi. Hivyo unapokutana na mtu wa aina hii basi umeumia, Unaweza kuona umekosea na huwezi kuonekana kuwa hujui lolote.

Watu wa aina hii hata ukimwambia, I MISS YOU…! Utasikia: kheeee! Leo umejifunza wapi?

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.