TUNAPOELEKEA 2017, HII INAKUHUSU KUTOKA KWA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Rais wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wote kuutunza na kuudumisha umoja katika mwaka 2017 huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii.
Rais Magufuli amendika maombi hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo pamoja na kuwaomba Watanzania kutekeleza mambo hayo amewatakiwa Watanzania heri ya mwaka mpya.
“Ombi langu kwa Watanzania wote tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA,” aliandika Rais Magufuli.
Ombi langu kwa Watanzania wote tuulinde,tuutunze na kuudumisha umoja wetu ktk mwaka 2017 kwa kufanya kazi kwa bidii. MUNGU IBARIKI TANZANIA.— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) December 27, 2016
Watanzania wenzangu,tukiwa tunakaribia kuumaliza mwaka 2016,naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya 2017.— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) December 27, 2016
No comments:
Post a Comment