FRIDAY XO : MAMBO MATANO MAKUBWA YANAYOPELEKEA USALITI KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI



FRIDAY XO 
kitu kinachoumiza kwenye mapenzi ni wenza kusalitiana, kwa mtu anaingia kwenye mapenzi akiwa anaimani kuwa mpenzi wake anampenda kwa dhati, swali la kujiuliza ni mambo gani ni kichocheo cha usaliti, fuatana nami katika makala hii.

>> Kutokuvutia tena
Moja ya sababu iliyopelekea kukubali kuoa au kuolewa na huyo mwenzi wako, kuna baadhi ya vitu ulivutiwa navyo ndio akawaacha wote na kumchagua huyo.  Vitu hivyo usipovizingatia na kuvi “maintain” vitasababisha hali ya kukinai kwa mwenzi wako na mwisho kuanza kuvutiwa na wengine kule nje.

>>> Mabadiliko mbalimbali ya kimaumbile mfn: Unene

Kila mwanandoa ana “test” yake ya mvuto kwa mwenzi wake, Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya wembamba wako sasa unapojiachia na kuwa mnene ila hamu ya kuendelea kuvutiwa nawe inapungua na baadaye inakwisha na kusababisha aanze kuchungulia nje.

• Kuna mwingine alikupenda kwasababu ya unene au kujazia katika maeneo Fulani Fulani. Sasa mwili ukiporomoka unapoteza ule mvuto tena na kumfanya apoteze hamu ya kuwa na wewe na kumfanya kuanza kuchungulia chungulia nje.

• Ni vizuri kujali afya yako na kujua ni vitu gani vinavyomvutia mwenzi wako kutoka kwenye mwili wako na ujitahidi kuvitunza “maintain” ili kuendelea kudumisha ule mvuto kwa mwenzi wako.

>>> Kutokwenda na wakati haswa katika mavazi.

Hili hasa ni kwa wanawake, Kabla ya kuolewa ulikuwa unajitahidi sana kujilemba na kujitunza kila wakati ulikuwa safi na nadhifu. Mumeo kila akikuangalia mpaka haamini kama ni wewe aliyekuoa ukiwa mrembo na wa kuvutia, Unavaa nguo nzuri tu pale unapotoka kwenda kanisani au mtoko maalumu.

>>Kukosekana kwa mawasiliano, 

Mawasiliano yana husisha pande zote mbili kwa anayetoa na anayepokea, mathalani katika vitu vya kawaida kama kujuliana hali pindi mnapokuwa mbali hasa wakati wa kutimiza majukumu ya kila siku, mfano meseji ya kumuuliza mwenza wako ameshindaje na anaendelea vipi katika utekelezaji wa majukumu yake, hali ikibadilika humfanya mwenza kufikiria tofauti na kuona humjali hatimaye kuwa msaliti.

>>>Kushindwa kuendeleza yale yanayompendeza kila mmoja wenu.Mnakubaliana mipango kama wanandoa lakini utakelezaji unakua mgumu, Mmoja anakuwa tayari kutekeleza na mwingine anashindwa.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.