TCU YATOA UFAFANUZI JUU YA SINTOFAHAMU WAOMABAJI WA VYUO VIKUU NCHINI 2016/2017


Image result for tanzania commission for universities images

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imetoa ufafanuzi juu ya taarifa za kutoka kwa matokeo ya waombaji wa nafasi za kujiunga na vyuo vikuu hapa nchini, kwa mwaka wa masomo 2016/2017

Kwa siku tatu sasa, kumekuwepo na taarifa za TCU kutoa matokeo ya nafasi hizo huku wanafunzi wengi wakilalamikia kushindwa kuyaona matokeo hayo katika tovuti ya tume hiyo.

Akizungumza kwa njia ya simu, Edward Mkaku, afisa habari mwandamizi wa TCU amesema, TCU tayari imeweka matokeo ya awali ya nafasi hizo lakini matokeo hayo ni awali tu na siyo rasmi mpaka pale yatakapothibitishwa.

Edward Mkaku, afisa habari mwandamizi wa TCU
Edward Mkaku, Afisa habari wa TCU

“Tumetoa matokeo ya awali (provisional results), ambayo mwanafunzi anatakiwa kuingia katika akaunti yake ya TCU na kuona kama amepangiwa Chuo au la, lakini matokeo hayo siyo rasmi mpaka pale yatakapokuwa yamethibitishwa (approved),” amesema Mkaku  na kufafanua zaidi kuwa;

“Katika matokeo ya sasa tuliyotoa, mwanafunzi hawezi kuona amepangiwa chuo gani wala kitivo au taaluma aliyopangiwa kusoma, ila tu anajulishwa kuwa amepangiwa kusomea kitu kimoja kati ya vile vitano alivyoomba.”

Akitolea ufafanuzi juu ya wanafunzi ambao wamekosa nafasi za kuchaguliwa katika hatua ya sasa, Mkaku amesema wanafunzi hao wanayo fursa ya kuomba tena nafasi hizo.

“Tayari zoezi la kuomba vyuo kwa awamu ya pili limeanza tangu Jumatatu, wanafunzi waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza wanaweza kuomba tena katika awamu hii ya pili,” amesema.

Uombaji wa nafasi kujiunga na vyuo vikuu unaofanyika mwaka huu, utakuwa chini ya vigezo vipya vya kujiunga na elimu ya ngazi hiyo tofauti na miaka iliyopita. Hii ni kufuatia mabadiliko yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chini ya Profesa Joyce Ndalichako.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.