MAGAZETI YA UINGEREZA YALICHOANDIKA KUHUSU MKOSI UNAOMPATA ROONEY KATIKA MAISHA YAKE YA SOKA KWA SASA
Tayari Rooney ameshapoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha Manchester United sasahivi anapanda mlima mwingine kuhakikisha anatetea nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England lakini amejikuta kwenye wakati mgumu kwa kuwa nahodha wa taifa lake anayezomewa na mashabiki wa nchi yake huku wakati huohuo si chaguo la kwanza tena pale Old Trafford.
Kocha wa muda wa England Gareth Southgate aliamua kuendelea kumtumia Rooney kama nahodha wake kwenye mechi nne akiwa kama kocha England licha ya Wazza kuwa katika kiwango cha chini kwa siku za karibuni huku akimwanzisha katika nafasi ya kiungo wa ulinzi wakati wa mchezo uliopita dhidi ya Malta.
Rooney alizomewa na mashabiki wa England kwenye uwanja wa Wembley ambao walionesha kutomuunga mkono kwenye mechi dhidi ya Malta.
Eric Dier akiwa ameitwa kwenye kikosi cha England kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Slovenia, Rooney huenda akawa kwenye wakati mgumu zaidi kwenye timu yake ya taifa.
Kwa sasa hapewi tena fursa ya kucheza mbele kwenye nafasi yake kama ilivyozoeleka nafasi ambayo amecheza kwa muda mrefu wa maisha yake ya soka lakini kwa sasa amerudishwa chini sehemu ambayo huenda inamsumbua.
Kiungo wa Spurs Eric Dier anaonekana kufit zaidi kwenye nafasi ya Rooney kitu ambacho kinasababisha presha kubwa kwa Southgate kumpiga chini nahodha wake.
Kwa mujibu wa kurasa za magazeti ya England, Southgate amesema hahofii kumtema Rooney.
No comments:
Post a Comment