KUTANA NA MWANAUME ALIYEISHI NA KISU TUMBONI KWA MIAKA 18

surgical scissors

Madaktari nchini Vietnam wametoa mkasi wa kufanyia upasuaji kutoka kwenye tumbo la mwanamume mmoja baada ya kukaa na mkasi huo kwa miaka 18.

Wataalamu wa upasuaji walisafiri kwa ndege kutoka mji mkuu wa Hanoi kusaidia katika upasuaji huo uliofanyika katika mkoa wa Thai Nguyen kaskazini mwa nchi hiyo

Mgonjwa huyo wa umri wa miaka 54 alifika hospitalini baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani mwezi uliopita. 
Lakini baada yake kupigwa picha ikagunduliwa kwamba alikuwa na kifaa cha chuma chenye ncha kali sehemu ya kushoto tumboni.
Alipimwa tena katika hospitali iliyo karibu katika mkoa jirani wa Bac Kan na ikabainika bila shaka kwamba alikuwa na mkasi wa urefu wa sentimita 15 (inchi 6) karibu na utumbo wake mkubwa, gazeti la Tuoi linasema.
Ma Van Nhat anasema huenda mkasi huo uliachwa mwilini mwake alipofanyiwa upasuaji katika hospitali kuu ya mkoa wa Bac Kan mwaka 1998 baada yake kuhusika katika ajali nyingine ya barabarani, kwa mujibu wa gazeti la Vietnam Express.
Hakuwa amepata tatizo lolote la kumfanya agundue alikuwa na kifaa hicho tumboni ila majuzi tu alipoanza kuhisi maumivu makali tumboni.
Alijaribu kunywa dawa za kutuliza maumivu lakini uchungu huo haukuisha.
Wataalamu waliomfanyia upasuaji kwa muda wa saa tatu walisema mkasi huo uliokuwa umeshika kutu baadhi ya sehemu zake ulikuwa umekwama na kushikana na baadhi ya viungo tuu. 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.