Arsenal wakaribia kumnasa mfungaji bora

ARSENAL WAKARIBIA KUMNASA MFUNGAJI BORA



Hivi karibuni kocha wa washika bunduki wa london mzee arsene wenger alinukuliwa akisema juu ya umuhimu wa kuimarisha scouting system ya arsenal,ambayo kwa miaka ya karibuni imeonekana kushindwa kufikia malengo yake kwa kuzembea kufanya uharaka wa kusajili wachezaji wanaochipukia, licha ya kuweza kuwaona mapema akitolea mfano wa wachezaji kama griezman na kante. 

Pengine somo limewaingia watu wa idara ya scouting ya arsenal,ripoti zinaonyesha arsenal wako kwenye hatua nzuri ya kumalizana na mfungaji bora wa ligi kuu ya ubeligiji,Kutokea Nigeria Henry Onyekuru mwenye umri wa miaka 19,aliyefunga magoli 20 msimu huu unaomalizika akichezea klabu ya KAS UPEN.

Mchezaji huyo ambaye inasemekana ana kipengele chenye kumruhusu kuama klabu hiyo endapo team itaweza kutoa dau la pauni za kiingereza 6.8,anatajwa kufuatiliwa kwa karibu na vilabu vya Everton na celtic japo arsenal wanaonekana kua kwenye nafasi kubwa ya kuweza kumnasa.

Pengine huu sio aina ya usajili ambao wapenzi na wanazi wa arsenal wanaonekana kufurahia,hasa kutokana na timu kushindwa kushinda mataji makubwa kwa miaka ya karibuni na mbaya zaidi msimu huu wamemaliza nje ya top four kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.

Pengine hii ni one for the future,na usajili haswa kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa magoli katika klabu ya Arsenal unakuja,bado kuna miezi mingi kabla ya dirisha la usajili kufungwa.



No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.