JARIBIO LA NUKLIA LA KOREA LALETA MAJANGA



Korea Kaskazini imefanya jaribo la sita la nyuklia kwa siri hii ni  kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya Japan.

Serikali nchini Japan imethibitisha kuwa Korea Kaskazini ilifanya jaribio la nyuklia kwa siri baada ya kutathmini taarifa kuto kwa idara ya hali ya hewa nchini humo na taarifa zingine.
Taarifa kutoka katika kituo cha Tv cha taifa cha Korea Kaskazini, zinasema kuwa serikali  itatoa tangazo muda mfupi baadae kuhusu jaribio hilo la makombora ya nyuklia.
Watabiri wa hali ya hewa mapema jana walitambua tetemeo dogo la ardhi, eneo ambapo Korea Kaskazini imefanyia majaribio ya nyuklia.
Tetemeko hilo dogo lilitokea saa kadhaa baada ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kupiwa picha akiwa na kile ambacho vyombo vya habari vilisema kuwa lilikuwa ni aina mpya ya bomu la hydrogen.
Japan imesema tetemeko hilo la ardhi limetokea baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio ka siri la silaha za nyuklia.
Ripoti za awali kutoka idara ya hali ya hewa ya Marekani zilitaja tetemeko hilo kuwa la ukubwa wa 5.6 lakini baadaye wakasema kuwa ukubwa huo ni wa 6.3 katika vipimo vya richta.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.