RYAN GIGGS AMUONYA JOSE MOURINHO

 RYAN GIGGS AMUONYA MOURINHO KUHUSU UNITED

Screen Shot 2016-03-30 at 4.33.18 PM

Jina linalotajwa sana kurithi mikoba ya LVG ni Jose Mourihno na kinachosubiriwa sasa hivi ni kutangazwa rasmi mwisho mwa msimu huu kama mambo yakienda kama inavyodhaniwa.
Licha ya kuwa na perfomance mbovu akiwa anaiongoza club ya Manchester United, lakini LVG hawezi kusahaulika kwa kitu alichofanya ambacho ni kuwapa nafasi vijana kutoka kwenye academy ya Manchester United.
Ryan Giggs amefurahishwa na kitu hicho na kusema maneno ambayo ni kama onyo kwa kocha anayekuja Manchester United kuchukua kazi ya LVG. Giggs amesema, “Hii imekua ni sehemu ya historia ya timu yetu. Tofauti na club nyingine hapa tuna utaratibu kwa kukuza wachezaji wetu na kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia. Japokua tunaweza kuleta wachezaji wa level hiyo lakini lazima tuwe na foward, winger au hata beki ambae ana kiwango cha dunia na ametokea hapa hapa Manchester. Mashabiki wanapenda na wanataka kuona wachezaji wanapitia katika njia hii ya kwetu na wanaipa heshima yake. Hivyo basi watoto hawatakiwi kusahaulika kwenye mfumo wa timu”.
alisema Ryan Giggs 

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.