DIAMOND PLATNUMZ ANAPANIA Hii 2016....
HII HAPA LIST YA WATU MAARUFU WANAO MILIKI GARI ANALOTAKA KUNUNUA DIAMOND 16'.
By JesseTM |
Siku zinazidi kusogea toka mwaka 2016 uingie, robo ya mwaka tumeshaimaliza ila February 1 2016 msanii Diamond Platnumz akiwa katika exclusive interview na Millard Ayo alithibitisha kuwa mwaka 2016 atanunua gari la kifahari aina ya Rolls Royce. Kwa kawaida Rolls Royce thamani yake hufikia milioni 500 za kitanzania.
Platnumz alimwambia Millard Ayo >>> ‘Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida’'
Kutokana na kuwa na bei kubwa Rolls Royce sio gari ambazo hutumiwa na watu wengi, March 31 hii hapa list ya baadhi ya watu marufu duniani ambao wanamiliki Rolls Royce.
Justine Bieber ameingia kwenye list hii kutokana na kumiliki Vintage Rolls Royce
Jay Z na Beyonce wapo katika list ya mastaa wa dunia wanaotembelea Rolls Royce. Jay Z na Beyonce wanatumia Rolls Royce Convertible.
Kim Kardashian na Kanye West wapo kwenye hii list kwa kumiliki Rolls Royce yao yenye rangi nyeusi.
Emmanuel Adebayor ambae anaeichezea Crystal Palace ya Uingereza yupo katika list ya baadhi ya mastaa wanaotembelea Rolls Royce, yeye kaiwekea namba zake binafsi za usajili yaani SEA maana yake Sheyi Emmanuel Adebayor.
Koffi Olomide huyu ni nguli wa muziki wa dansi kutokea Kongo, inaripotiwa alinunua Rolls Royce Phantom V12 6.7 mwaka 2013 kama zawada kwa mkewe ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka 20.
Hii hapavideo ya rolls royce on road.....
Hao ndo watu wanaomiliki gari hilo la kifaharii ambalo wanalo wahache kutokana na ughali wali.. best wishes Diamond.
No comments:
Post a Comment