LEO KATIKA HISTORIA.. 06 APRIL.
TODAY IN HISTORY.. APRIL 06
Siku kama ya leo miaka 50 iliyopita, kufuatia kujiri upinzani na mapambano ya wananchi Waislamu wa Iran
,Imam Khomeini mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliachiliwa huru kutoka jela. Imam Khomeini alitiwa mbaroni na maafisa wa usalama wa utawala wa Shah, baada ya hotuba yake iliyofichua njama za utawala huo. Hata hivyo baada ya kutiwa mbaroni Imam Khomeini, kulishuhudiwa maandamano na upinzani mkubwa huku wananchi hao wa Iran wakitaka kuachiliwa huru kwa kiongozi wao huyo. Upinzani huo uliulazimisha utawala wa Mfalme Shah umuachilie huru Imam Khomeini.
Siku kama ya leo miaka 20 iliyopita, vita vya umwagaji damu mkubwa kati ya makabila mawili ya Watutsi na Wahutu vilianza nchini Rwanda. Katika vita hivyo Wahutu wenye misimamo mikali wa Rwanda waliwaua zaidi ya watu laki nane kutoka kabila la Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani na zaidi ya watu milioni mbili kuwa wakimbizi. Tofauti kati ya makabila hayo mawili, zilianza makumi ya miaka kabla ya hapo na kwa mara kadhaa zilisababisha mauaji dhidi ya watu wasio na hatia. Wahutu wanaunda asilimia 84 ya jamii ya Rwanda na kabila hilo lilikuwa madarakani hadi mwaka 1994.
Pia nimekusogezea moja ya video zinazoenesha historia ya leo hapa
Pia nimekusogezea moja ya video zinazoenesha historia ya leo hapa
Siku kama ya leo miaka 29 iliyopita Ja'far Nimeiry, Rais wa zamani wa Sudan alipinduliwa na Jenerali Abdulrahman Swarul-Dhahab aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo. Ni vyema kuashiria hapa kuwa, Nimeiry aliingia madarakani baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Sudan mnamo mwaka 1969. Nimeiry aliongoza Sudan kimabavu kwa miaka 16 na kuanzisha uhusiano mkubwa kati ya nchi hiyo na Marekani.
Na siku kama ya leo miaka 434 iliyopita, ardhi ya Ureno moja kati ya nchi zilizokuwa na nguvu barani Ulaya katika karne za 15 na 16 iliunganishwa na Uhispania. Ureno ilikuwa mpinzani wa kisiasa na kikoloni wa Uhispania huko Asia, Afrika na Marekani. Hata hivyo kutokana na raia wa nchi hiyo kuhamia kwa wingi katika nchi makoloni ya Ureno na vile vile hali mbaya ya kiuchumi taratibu Ureno ilianza kupoteza satwa na nguvu yake ya kisasa. Udhaifu na kutokuwa na nguvu Ureno uliipelekea Uhispania kuivamia nchi hiyo. Pamoja na hayo yote hatimaye mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Ureno ya mwaka 1640 yalipelekea kukombolewa tena nchi hiyo
No comments:
Post a Comment