REAL MADRID, BBC WANAKIBARUA KIZITO FAINALI ULAYA
REAL MADRID KUUONDOA MKOSI WA MIAKA 29 KUFUZU NUSU FAINALI ULAYA : KIBARUA KIZITO BBC.
12 April 2016.By Shaffidauda
Kipigo cha kushtua kutoka Wolfsburg kilifikisha tamati rekodi ya Madrid kutopoteza mechi hata moja katika michuano ya ulaya msimu huu, na itawabidi wacheze na kufanikiwa kulipa deni la 2-0 kwa mara kwanza tangu mwaka 1987
Itakuwa ni ujinga kuondoa kabisa uwezekano wa wa Madrid kupindua matokeo katika mchezo wa pili na kusonga mbele kwenda nusu fainali, lakini ili kufanikiwa kufanya hivyo Los Blancos itabidi waondoe mkosi unaowaandama kwa miaka 29.
Magoli kutoka Ricardo Rodriguez na Max Arnold yaliwapa ushindi wa 2-0 Wolfsburg katika mchezo wa kwanza, na wajerumani walistahili kushinda baada ya Madrid kuonyesha kiwango kibovu.
Kipigo hicho kimewaacha vijana wa Zinedine Zidane wakiwa na changamoto ya kulipa deni la magoli na kwenda kushinda – jambo ambalo mara ya mwisho walifanikiwa kufanya mwaka 1987. Ilikuwa katika robo fainali ya michuano ya ukaya, vs Red Star Belgrade ambapo walifungwa 4-2 ugenini.
Hugo Sanchez alifunga magoli mawili nchini Yugoslavia na magoli hayo yakiwasaidia Madrid kufuzu baadabya kwenda kushinda 2-0 Santiago Bernabeu kwa magoli ya Emilio Butragueno na Manuel Sanchis.
Leo hii Ronaldo na wenzake watahitaji kuumaliza mkosi wa kushindwa kubadili matokeo kama ilivyokuwa kwa akina Hugo Sanchez 1987.
Kipigo cha Madrid juzi, kinamaanisha kwamba Barcelona ndio imebaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote katika Champions League msimu huu.
No comments:
Post a Comment