NEWS UPDATES: KOREA KASKAZINI KULIPUA BOMU LA NYUKLIA

Korea Kusini imesema imepata dalili kwamba Korea Kaskazini inajiandaa kufanya jaribio la tano la bomu la nyuklia, Rais Park Geun-hye amesema. By Jesse Ngoty on 18 April 2016
Hakufafanua zaidi kuhusu dalili hizo, lakini ameagiza jeshi la nchi yake kuwa tayari, shirika la habari la nchi hiyo limesema.
Kumekuwa na ripoti katika vyombo vya habari nchini Korea Kusini kwamba kumeongezeka shughuli katika kituo cha majaribio ya silaha za nyuklia cha Korea Kaskazini cha Punggye-ri, ambapo majaribio ya awali yalitekelezwa.
Iwapo Pyongyang itaendelea na kufanyia majaribio bomu la nyuklia, basi itakuwa ni kukaidi zaidi vikwazo vikali ilivyoongezewa na Umoja wa Mataifa mwezi jana.
"Tupo katika hali ya kutatanisha, hatujui iwapo Korea Kaskazini inaweza kufanya uchokozi kama njia ya kujitetea kutokana na kutengwa na jamii ya kimataifa na pia kuimarisha uungwaji mkono ndani ya nchi,” Bi Park aliambia maafisa wake wakuu wa jeshi, shirika la habari la Yonhap liliripoti.
Mwezi Januari, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la nne la silaha za nyuklia na baadaye ikarusha kombora baharini.
Image copyrigh
Image capt
Hatua hiyo iliongeza hali ya wasiwasi katika rasi ya Korea.
Waangalizi wanasema huenda jaribio hilo la bomu likafanywa kabla ya mkutano mkuu wa chama tawala cha Workers' Party mjini Pyongyang mwezi Mei.
Wataalamu wanaamini Korea Kaskazini haina uwezo wa kiteknolojia wa kuweka silaha ya nyuklia kwenye kombora, ingawa imepiga hatua kubwa katika mpango wake wa nyuklia miaka ya karibuni.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.