TONIGHT., LIVERPOOL VS DORTMUND QUARTER FINAL UEFA EUROPA LEAGUE

SPORTS


DORTMUND VS LIVERPOOL: KLOPP ATAWEZA KUTEGUA BOMU ALILOLITEGA MWENYEWE?





Pambano kali linasubiriwa pale Ujerumani kwenye uwanja wa Signal Iduna Park usiku wa leo kati ya miamba ya soka la Ujerumani Borussia Dortmund dhidi ya Liverpool ikiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya UEFA Europa League (UEFA ndogo).
Liverpool wamekuwa na matokeo mazuri kwenye michuano ya Europa League hadi sasa huku kiwango chao bora kwenye msimu huu walikionesha kwenye michezo miwili dhidi ya Manchester United raund iliyopita.
Mchezo dhidi ya Dortmund ni moja kati ya michezo migumu ambayo Liverpool inakutana nayo kutokana na timu hiyo kuwa kwenye kiwango cha juu duniani kwa sasa wakiwa wameshajihakikishia ticket ya kucheza michuano ya Champions League msimu ujao kutokana na kuwa kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Bundesliga.
Safu ya ushambuliaji ya Dortmund imekuwa hatari zaidi na inashangza ni kwanini kikosi hicho kinakosekana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Bila shaka hata kidgo kikosi cha Thomas Tuchel kinapewa nafasi kubwa ya kunyanyua ndoo ya Europa League msimu huu.
Urejeo wa Jurgen Klopp kwenye uwanja wa Signal Iduna Park unatarajiwa kuibua hisia tofauti kwa mashabi wa Dortmund lakini bado mchezo huo utakuwa ni mkubwa na mgumu kwa Liverpool.
Dortmund iliitupa Spurs nje ya mashindano kwenye mchezo ambao Mauricio Pochettino aliwapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza na kujikuta akipokea kichapo cha nguvu na kuyaaga mashindano hayo.
Mats Hummels, Sokratis Papastathopoulos pamoja na Ilkay Gundogan walifanya mazoezi jana na wanatarajiwa kuwemo kwenye kikosi kitakachoikabiloi Liverool.
Dortmund wanatarajia kupambana na Schalke kwenye mchezo wa derby utakaopigwa Jumapili ya mwisho mwa juma hili hivyo Gundogan anawezakupumzishwa kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.
Kwa upande wa Klopp yeye huenda akampumzisha Daniel Sturridge na kumuanzisha Divock Origi ambaye anaonekana kuwa fit kwa sasa.
Philippe Coutinho pamoja na Roberto Firminowako fit, Klopp anaamini atarejea Anfield akiwa na uhakika bado kikosi chake kinanafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano.
Kikosi cha Borussia Dortmund kinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo: Roman Weidenfeller, Lukasz Piszczek, Mats Hummels, Matthias Ginter, Marcel Schmelzer, Julian Wiegl, Sven Bender, Gonzalo Castro, Henrikh Mkhitaryan, Marco Reus na Pierre-Emerick Aubameyang.

Kikosi cha Liverpool kinatarajiwa kuwa na wachezaji wafuatao: Simon Mignolet, Nathaniel Clyne, Dejan Lovren, Mamadou Sakho, Alberto Moreno, Emre Can, Jordan Henderson, James Milner, Philippe Coutinho, Roberto Firmino pamoja na Divock Origi.



Sources: Shaffidauda.com
               goal.com
               skysports
              

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.