UEFA QUATER FINAL, TONIGHT BARCELONA VS ATLETICO MADRID.
BARCELONA WATAWEZA
KUENDELEZA REKODI YAO
YAKUFUNGA? KAZII KWA MSN
USIKU WA LEO
Ni wazi kwamba ikiwa Barcelona watafanikiwa kufunga leo usiku katika uwanja wa Vicente Calderon, itakuwa hatua kubwa katika kuelekea kufuzu.
Sio tu kwa sababu itawabidi Atletico kufunga magoli 3 ili kushinda – au mawili ili mechi iende muda wa ziada – bali kwa sababu kwa Barca kufunga, itawalazimu Atletico waende mbele zaidi kutafuta goli, kitu ambacho sio mchezo wao wa kawaida.
Baada ya kushindwa kupata goli vs Real Sociedad, takwimu zinaonyesha itakuwa vigumu kukosa goli pale Calderon. Rekodi zinaonyesha Barcelona kwa miaka 8 iliyopita hawajawahi kutokufunga goli katika mechi 2 mfululizo.
Mara ya mwisho jambo hilo limetokea ilikuwa msimu wa 2008-09. Vijana wa Pep Guardiola walifungwa 1-0 na Wisla Krakow na wakaja kufungwa tena na Numancia 1-0 mchezo uliofuatia.
Barani ulaya, Barcelona wamefanikiwa kufunga mfululizo kwa miaka miwili. Mara ya mwisho kushindwa kufunga ilikuwa katika uwanja wa Vicente Carlderon vs Atletico katika robo fainali ya msimu wa 2013/14. Kutokea hapo Barca wamefanikiwa kufunga mara 22 mfululizo katika michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment