ALIKIBA KALA SHAVU - SONY MUSIC --- TUNAKUTAKIA HERI KUTUWAKILISHA VYEMA TANZANIA KIMATAIFA.

13261070_1578220049138060_345601967_n
Staa huyo leo amesaini mkataba na record label hiyo kubwa duniani jijini Johannesburg, Afrika Kusini. “Ni step moja wapo watu wangependa kuniona na leo ndio imefikia,” alisema Kiba mbele ya waandishi wa habari waliokuwa wamehudhuria kwenye utiaji saini katika deal hilo.”
“Niliwaambia nitafika sehemu mtaridhika na ninachokifanya. Naona hii support imetoka kwa mashabiki, nawapenda, mtanisamehe kama ntakuwa nimewakosea, kiukweli sote ni binadamu,” aliongeza.
“Ilikuwa kati ya ndoto zangu, nitafanya party kwaajili yao, kuwaona, kufurahia pamoja nao wanaopenda maendeleo yangu. Naombeni niwashukuru sana, nina imani kwamba ni malengo mazuri ninayoyalenga, na in the future ntaendelea kufanya kitu kama nilichofanya leo, nina imani mna furaha kama niliyonayo leo,” alisisitiza.
Kwenye hafla hiyo video nne za nyimbo zake zilichezwa zikiwemo Mwana, Chekecha Cheketua, Nagharamia, Lupela, Unconditionally Bae na Aje.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.