KILICHOPELEKEA MSUKUMA KUSEMA ASILIMIA KUBWA YA WABUNGE WALIENDA KWA WAGANGA



Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku (Musukuma) amesema kuwa wabunge wengi ndani ya Bunge la Tanzania wamepita kwa waganga wa kienyeji kipindi cha uchaguzi huku akisema kama kuna ambao hawajapita ni wawili au watatu.

Mheshimiwa Kasheku ameyasema hayo alipokuwa akichangia hoja ya Wizara ya Habari kuwa wasanii wanatumiwa wakati wa uchaguzi lakini baada ya uchaguzi wanatelekezwa bila msaada wowote.
“Muheshimiwa Spika, kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia wabunge wanalalamika na kuwatetea sana wasanii pindi wanapopata matatizo, kwamba tunawatumia katika chaguzi alafu baada ya chaguzi hatuwasaidii, lakini Muheshimiwa Naibu Spika waganga wa Kienyeji kwa karama niliyonayo, nikiangalia humu ndani wawili watatu wakati wa uchaguzi wawili watatu hamkupita kwao, wawili ama watatu labda mzee Thelathini .
Muheshimiwa Spika lakini si tu hawa wabunge na jamii nzima ,na baada ya uchaguzi tunawatelekeza na kuwatumia Polisi, “Je, Mheshimiwa Spika, serikali haioni umuhimu wa kujenga chuo cha kuwasaidia waganga hawa hata kama ni kwa elimu ndogo? aliuliza Kasheku.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.