CHELSEA WAZIDI KUUKARIBIA UBINGWA WA EPL, NYOTA WAKE WAZIDI KUZIKARIBIA REKODI



Ushindi wa Chelsea katika mchezo wao dhidi ya Southampton umewapa jumla ya alama 78 ambazo katika historia ya Epl ni timu moja tu ambayo ilishawahi kupata alama 78 au zaidi katika mechi 33 na kukosa ubingwa.
Timu hyo ilikuwa Manchester United ambapo katika msimu wa 2011-2012 walipata alama 78 lakini wakishuhudia ubingwa ukaenda kwa majirani zao Man City, Chelsea chini ya Conte wanaonekana hawataki hili liwatokee.
Bado michezo mitano katika ligi ya Epl lakini katika michezo hiyo Chelsea watahitaji kushinda michezo minne ili kutawazwa mabingwa wapya wa ligi hiyo, hii ikiwa na maana Chelsea kuanzia sasa wanahitaji alama 12 tu ili kuwa mabingwa wa Uingereza.
Katika mchezo kati ya Chelsea na Southampton kuna rekodi zilitokea na kukaribia kuvunjwa moja wapo ikiwa ile ya Jim Floyd Hasselbank ya kuwa mchezaji aliyefunga haraka zaidi mabao 50 katika historia ya Epl kwa kufunga ndani ya michezo 84.
Lakini Diego Costa amekuwa wa pili chinj ya Hassrlbank kwani magoli mawili aliyofunga dhidi ya Southampton yamemfanya kufikisha magoli 50 lakini yeye akiwa ametumia michezo 85 ukiwa ni mchezo mmoja zaidi ya Hasselbank.
Lakini Cesc Fabregas naye amekuwa mchezaji wa pili kwa kuwa na assist nyingi katika Epl ambapo hadi sasa Fabregas ana assist 103 ambapo ni mchezaji mmoja tu aliyemzidi, ambaye ni Ryan Gigs mwenye assist 162.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.