PICHA : KAMANDA MPYA WA CHADEMA, WEMA SEPETU ALICHOFANYA SIKU YA WANAWAKE



Kamanda mpya wa Chadema Wema Sepetu na mbunge wa viti maalum Morogoro Devota Minja amesherekea siku ya wanawake duniani kwa kupanda miti mkoani Morogoro.

Muigizaji huyo amedai upandaji wa miti utakuja kuwa tija kwa jamii hasa hasa kupunguza kero kubwa ya maji inayotukabili wanawake.
“Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji,” aliandika Wema Instagram.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.