UTAFITI : MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII HUSABABESHA UPWEKE

Related image

Mitandao ya mawasiliano ya kijamii kama vile Twitter, Facebook inasababisha watu wengi zaidi kuhisi wenye upweke , kulingana na wanasaikolojia wa Marekani.
Ripoti ya uchunguzi wao inasema kuwa masaa zaidi ya mawili ya matumizi ya mitandao ya kijamii kwa siku huongeza uwezekano mara dufu wa mtu kujihisi ametengwa na jamii
Ripoti hiyo ya wanasaikolojia inadai uwezo wa kupata mawazo ya maisha ya watu wengine unaweza kusababisha hisia za wivu.
Utafiti huo pia uliangazia watu wanaotumia mitandao ya Instagram, Snapchat na Tumblr.
Ni muhimu kukumbuka kuwa yale unayoyashuhudia katika mitandao ya kijamii si sababu muhimu ya kukufanya ujihisi vibaya -lakini inaweza kuwa sababu.
Yale unayoyashuhudia kwenye mitandao ya kijamii yanaweza kuchochea hisia ambazo tayari unazo.
" hatujatambua nini kinachokuja kwanza - matumizi ya mitandao ya kijamii ama dhana ya kuhisi umetengwa na jamii ," amesema Elizabeth Miller, profesa wa tiba ya watoto katika chuo kikuu cha Pittsburgh, ambaye ni mmoja waandishi wa utafiti.
" Inawezekana kwamba vijana ambao awali walihisi wametengwa na jamii walianza kutumia mitandao ya mawasiliano ya kijamii. Ama inawezekana kwamba kuongezeka kwa matumizi ya mitandao ya kijamii kulisababisha kwa kiasi fulani kujihisi wametengwa na dunia halisi."

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.