BORESHA AFYA YAKO KWA KULA VYAKULA VYA KUPUNGUZA SUMU MWILINI, NIMEKUSOGEZEA AINA YA VYAKULA HIVYO HAPA
VYAKULA VYA KUPUNGUZA SUMU NA MUWAKO WA SELI MWILINI (INFLAMMATION)
Leo katika upande wa afya, mtu wangu wa nguvu kakuandalia haya hapa... Boresha afya yako na lishe.
Vyakula tunavyokula kila siku ni msingi muhimu sana wa afya yetu. Uwezo wa mwili kupambana na magonjwa mbalimbali haujengwi na dawa, bali na aina ya vyakula tunavyokula. Kitendo cha muwako wa seli mwilini (inflammation), ambacho kinga ya mwili wako hushambulia vijidudu kama bakteria, kemikali za mimea kama poleni au kemikali za aina nyingine kutoka katika mazingira. Muwako huu wa seli za mwili husaidia kuulinda mwili dhidi ya magonjwa na kemikali zenye madhara kutoka katika mazingiara. Hata hivyo, uwakaji huu hutokea kwa muda mfupi na kisha kuacha.
Kuna wakati unatokea muwako huu wa seli unaendelea kwa muda mrefu zaidi ya kawaida, na hapa ndipo unapoleta madhara kwa mwili. Magonjwa mengi kama saratani, magonjwa ya moyo na kisukari huchangiwa kutokana na uwakaji wa seli kwa muda mrefu (chronic inflammation)
Vyakula Vinavyochangia Muwako wa Seli
Kuna vyakula ambavyo huongeza muwako wa seli na hivyo kuchangia kutokea kwa magonjwa haya. Nafaka zilizokobolewa, vyakula vya kukaanga, soda na nyama za kusindika ni mojawapo ya vyakula ambavyo huchangia magonjwa haya kutokea. Kwa ujumla, vyakula ambavyo sio vizuri kwa afya huwa na kemikali ambazo husababisha muwako wa seli na kisha magonjwa kama saratani kutokea.
Vyakula Vinavyopunguza Sumu na Muwako wa Seli
Kuhakikisha kwenye mlo wako unapata vyakula ambavyo havina ua hupunguza sumu mwilini ni muhimu ili kuzuia kutokea kwa magonjwa kama saratani au kisukari. Vyakula vifuatavyo hupunguza muwako wa seli za mwili;
- Nyanya
- Mafuta ya zeituni
- Mboga za majani za kijani
- Nuts kama almond,walnut, korosho, karanga
- Samaki kama salmoni, tuna
- Matunda kama machungwa, zabibu, matofu, strawberries na cherries.
Vyakula hivi vina kemikali za kuondoa sumu (anti-oxidants) kwa wingi ambazo huondoa sumu (free-radicals) zinazoleta muwako wa seli.
Mabadiliko Zaidi Katika Mlo Wako
Kunguza sumu na muwako wa seli mwilini, jitahidi kuwa na mlo wenye virutubisho vingi kwa wingi. Mlo wenye matunda kwa wingi, mboga za majani, nuts kama karanga, korosho, nafaka zisizokobolewa, samaki na mafuta ya mimea. Mlo wa aina huu utakusaidia pia kudhibiti uzito wa mwili wako nakukufanya ujisikie vizuri.
Pamoja na kupunguza sumu mwilini, vyakula vya asili ambavyo havijasindikwa husaidia kuimarisha afya yako kimwili na kisaikolojia.
No comments:
Post a Comment