MAMBO 8 YANAYOWEZA HATARISHA MAHUSIANO YAKO YA KIMAPENZI.

 FRIDAY X
MAMBO 8 YANAYOWEZA HATARISHA MAHUSIANO YA KIMAPENZI, USIYAWAZE WALA KUYAFANYA HAYA KUDUMISHA MAHUSIANO. 
Na Gwakisa Kalumbeta. 




Naomba nikuulize wewe mwenzangu ambaye upo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye unahisi ndiye sahihi kwako, ghafla unaingiwa na hisia ambazo katika mapenzi zinakuwa zinauweka uhusiano wako rehani, Je unazifahamu hisia ambazo ni hatarishi kwako karibu katika uwanja wa Mtembezi Mahaba na mie somo wako nipo tayari kukujuza.
1. NASALITIWA 

Kuishi katika mapenzi huku ukiwa na fikra kwamba mwenza wako anakusaliti ni jambo baya kwa vile huathiri msukumo wa ndani wa kupenda. Matokeo yake utajikuta ukishindwa kutimiza wajibu wako ama mke/mume kwa sababu tu ya kuendekeza hisia mbaya, acha kuhisit afuta ukweli.
2. TUTAACHANA

Kuna wapenzi ambao wanaishi na mawazo ya “ipo siku tutaachana”, Wanafanya hivyo eti kwa kutafsiri mwenendo usio ridhisha wa mapenzi yao, Kusema kweli hili ni jambo baya kwani huondoa ari na kujenga ufa wa mapenzi.
Huwafanya wapenzi kubakia na wazo moja tu, la kutafuta sehemu mbadala ya kwenda baada ya kuachana. Usiwaze kabisa kuachana hata kama mnagombana na mwenzako kila siku.
3. SIWEZI MAPENZI

Baadhi ya wapenzi huwa na hisia kwamba hawayawezi mapenzi,Hata kama hawaja ambiwa chochote kuhusu kuto watosheleza wenza wao faragha hivyo hukimbilia kujihukumu wenyewe wakati hujaambiwa kama echeza chini ya kiwango, hofu ya nini? Usiwaze hivyo, kama na lolote linalo kufanya uwe na hofu muulize mwenzio.
4. NINA KASORO

Naamini mitaani wapo watu ambao huamini wana kasoro fulani ndiyo maana hawafikii viwango vya kupendwa kama wanavyohitaji, “Yaani mimi ningekuwa kama fulani ningefurahi sana lakini ufupi wangu ndiyo tatizo.” Hizi ni hisia mbaya tu, kumbuka kuna wafupi wanapendwa ile mbaya, Jisahihishe na epuka kujishusha hadhi kwenye hisia zako.
5. NITAMUUA

Miongoni mwa hisia mbaya kabisa kwenye mapenzi ni kufikiria kumuua mwenzako kwa sababu yoyote, “Nikimfumania na mwanaume mwingine nitamuua.” Mtu anaye tawaliwa na mawazo ya aina hii anajiweka katika mtego mbaya kisaikolojia wa kuja kutekeleza kile anacho jiapiza hata kwa sababu ndogo, Usifikirie hivyo maishani mwako.
6. NIMEKOSEA KUCHAGUA

Usijihukumu makosa kwa sababu umeona mpenzi wako ana tatizo fulani. Fahamu kuwa kasoro ni sehemu ya ubinadamu. Weka mikakati ya kumuongoza mwezio kuliko kuhitimisha kwa mawazo kwamba ulikosea kumchagua. “Ningejua kama yuko hivi nisingemchagua.” Usiwaze hivi!
7. HATUWEZI KUZAA

Kuna wapenzi ambao kwa kuishi miaka mitatu au minne pamoja bila kupata mtoto hufikia kwenye fikra kwamba hawawezi kuzaa. “Mmm, mwaka wa nne umepita bila mtoto, nadhani sisi hatuwezi kuzaa.” Kwa nini msizae? Hizo ni fikra zako, hamjaambiwa na daktari sasa iweje uwaze hivyo? Jipe moyo kwani kuna watu walizaa baada ya miaka kumi, iweje ninyi wa mwaka mmoja?
8. UNANIDANGANYA

Ipo aina ya watu ambao hata kama wakiambiwa wanapendwa sana, hukimbilia kusema na kuamini kuwa wanadanganywa. “Mmm unanidanganya.” Atasema hivyo licha ya kuona mwanaume anavyojituma kumsotea na kumuonesha kila dalili za mapenzi. Hili ni jambo baya, ukithibitisha kwamba unapendwa usihisi unadanganywa, utapoteza bahati yako.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.