PICHA : BASI LATUMIKA KUFUNDISHIA MASOMO YA KOMPYUTA, LIMEJENGEWA MEZA ZENYE KOMPYUTA NDANI KATIKA VITI VYA ABIRIA

Basi

Katika ulimwengu wa sasa, huwa ni kama hitaji la msingi kijana kuwa na ujuzi wa kutumia kompyuta.
Ni ujuzi unaohitajika katika maeneo mengi ya kazi na hata katika kutekeleza shughuli za kila siku.
Lakini kwa vijana wengi ambao hukosa nafasi ya kujiunga na shule au vyuo vinavyotoa mafunzo ya kompyuta, huwa vigumu sana kupokea ujuzi huu.
Wengi hulazimika kulipia vyuo maalumu kupata fursa hii ilhali kwa wengine, kutokana na kazi wanazozifanya kila siku, huwa vigumu kupata muda.
Lakini wakfu wa shirika la Craft Silicon Foundation, unaomilikiwa na kampuni ya kuuza programu za kompyuta, umeanzisha mradi unaowawezesha vijana kujifunza kutumia komputa ndani ya basi ambalo ni darasa.
"Mimi natoka Kibera, kwa sababu nimejaribu kutafuta pesa ili niweze kujilipia masomo ya kompyuta. Kazi ninayoifanya mapato ni ya chini sana sijapata pesa ambazo zinaweza kunisaidia ili niweze kulipia masomo hayo," anasema mmoja wa wanafunzi hao, Wesley Soi.
"Masomo haya yamenisaidia sana."
Basi hilo huhudumia vijana maskini katika mitaa ya Kawangware, Mukuru, Korogocho, Kibera na Mathare, nchini Kenya. 
Basi

"Nilikuwa na shida mwenyewe pale nilipokuwa nikisoma. Nilikuwa na shida ya usafiri ndio maana nikazindua basi hili ili niweze kuwasaidia wengine wasipitie kile nilichopitia nilipokuwa mwanafunzi," anasema Priya Budhabhatti, mwanzilishi wa mradi huo.
"Nimeanza mradi huu kwa sababu wengine hawana karo ya kujiunga na taasisi mbalimbali na ndio maana basi hili litawafikishia elimu hadi mlangoni mwao,'
Masomo hayo hutolewa bila malipo.
Mwanafunzi
Wanafunzi


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.