TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA - 5/3/2018
Everton wanataka Arsene Wenger kuwa meneja wao ikiwa atafutwa na Arsenal. Mmliki wa klabu ya Everton Farhad Moshiri anaamini kuwa Wenger ni bora zaidi kuisaidia Everton kujijenga.
---------------
Chelsea wana mpango wa kumleta mchezaji wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta katika safu yake ya usimamizi.
Arsenal wanataka mrithi wa Wenger kuwa kocha mkuu badala ya meneja, hatua ambayo itampa fursa zaidi ya kufunza
-----------------
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry, anasema atakubanli ikiwa ataombwa kuchukua mahala pake Arsen Wenger.
----------------
Kiungo wa kati wa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, anasema lawama dhidi yake kwa kuhamia Anfield kutoka Arsenal ni upuzi akisema kuwa lawama hizo hazima athari yoyote kwake.
---------------
Mashambulizi wa Brazil Willian, 29, anasema anataka kusalia katika klabu hiyo ya Premier League licha Manchester United kuonyesha nia ya kumsaini
---------------
Tottenham wanamtaka mchezaji wa Bayer Leverkusen mlinzi raia wa Ujerumani Jonathan Tah, 22 kuchukua mahala pake Toby Alderweireld. Tottenham wameshindwa kuafikiana mkataba mpya na mchezaji huyo wa miaka 29.
--------------
Paris Saint-Germain hawatamuuza Neymar mwisho wa msimu, kwa mujibu wa mkurugenzi Antero Henrique, licha ya mchezaji huyo wa miaka 26 kuhusishwa na Real Madrid.
--------------
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema haelewi vizuri kuhusu kikosi watakutana nacho Jumatatu usiku cha Manchester United.
No comments:
Post a Comment