AMCHINJA MPENZI WAKE NA KUWEKA KWENYE BAJA LA MAJI



Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake... aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.