BAADA YA KIPIGO CHA AIBU, KUWENI NA SUBIRA, WENGER BADO HAJAFIKIRIA KUONDOKA ARSENAL

Image result for arsene wenger

Arsene Wenger amesema ataamua hatma yake kulingana na “picha kubwa” zaidi tu ya matokeo ambayo klabu hiyo inayopata kwa sasa na akakataa fikra za kuwa amejiweka katika wakati mgumu kwa kutokusaini mkataba mpya mapema.

Wenger mara kadhaa amekuwa kaisisitiza kuwa uamuzi wa yeye na hatma yake ya kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo atautoa mwishoni mwa msimu lakini kiwango kibovu cha siku za karibuni hasa kuanzia mwezi uliopita imeongeza idadi ya mashabiki inayomtaka kujiuzulu kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo.
Sanchez walks off at Arsenal
Arsenal wapo nje ya mbio za ubingwa huku wakiwa wametoka kupoteza dhidi ya Chelsea na Liverpool kwenye ligi kuu ya Uingereza huku pia wakiwa wamepoteza kwa mabao 5-1 dhidi ya klabu ya Bayern Munich kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya 16 bora.
Lakini Wenger, ambaye amekuwa klabuni hapo tangu mwaka 1996, amesema kuwa hali iliyopo klabuni hapo kwa sasa kwa maana ya matokeo mabovu haitokuwa sababu pekee ambayo ipo kichwani kwake.
Mashabiki wa Arsenal wabeba bango la kumtaka Arsene Wenger kuondoka
“Hufanyi maamuzi ya namna hiyo kwa kutizama matokeo ya mchezo mmoja au miwili mibovu uliyopitia” alisema Wenger. 
“Lazima utizame picha kwa ukubwa wake na kuona, je unaweza kuipeleka klabu hii katika hatua kubwa zaidi, au unaweza kufika katika hatua kubwa zaidi. Upo tayari kuwajibika kwa hayo yote?
“Lakini pia maamuzi haya hayawezi kuhusika na hizi wiki mbili tu katika miaka. Sijihisi kama nimewekwa katika wakati mgumu kabisa.”

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.