BREAKING NEWS: JENGO LAPOROMOKA NAIROBI, MTOTO WA MWAKA MMOJA NA NUSU ANUSURIKA




Mtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.

Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.

Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo. 

Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo. 

Baadhi ya wakazi wanasaidia kuwapelekea chakula watu waliohusika katika shughuli za uokoaji.

Katika nyumba jirani wakazi wanatazama waokoaji  wakiendelea na kazi ya uokoaji huku wasiwasi ukiibuka Kwamba muda  unayoyoma kwa watu ambao huenda bado wapo hai chini ya vifusi 

Idara mbalimbali nchini Kenya wakiwemo vijana kwa huduma ya Taifa  (NYS) linasaidia kudhibiti watu na katika uokoaji




Watu 96 bado hawajulikani walipo kufikia sasa. Juhudi za uokoaji zinaendelea.










No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.