MAKANISA KUWEKEWA WI-FI YA BURE UJERUMANI ... "GODSPOTS"

French Cathedral



22 May 2016    6:30 pm  

na Jesse Ngoty

Makanisa ya Kiprotestanti maeneo ya kati nchini Ujerumani yatakuwa yakiwapa waumini fursa ya kuingia katika mtandao, kwa kuwawekea huduma ya wi-fi bila malipo.

Huduma hiyo itapatikana katika maeneo ambayo, kwa kufuata ‘hostpots’ ambalo ni jina la vitovu vya huduma, yamepewa jina "Godspots".
Huduma hiyo ya Wi-fi itawekwa katika makanisa 220 katika majimbo ya Berlin na Brandenberg.
Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha RBB, mpango huo baadaye utatekelezwa katika makanisa 3,000
Makanisa ya kwanza kupata huduma hiyo yatakuwa kanisa kuu la French Cathedral eneo la Gendarmenmarkt na kanisa la Kaiser Wilhelm Memorial Church.
Watu wataweza kutumia huduma hiyo kutoka ndani nan je ya kanisa.
Wanaotumia huduma hiyo watalakiwa na ukurasa wa tovuti yenye maelezo kuhusu kanisa lenyewe, jamii na maelezo ya kidini.
Lakini baadaye, wataweza kuchakura chochote watakacho katika mtandao wote.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.