WHO: RWANDA YAONGOZA KWA MUDA WA KUISHI AFRIKA MASHARIKI, MIAKA 66 " LIFE SPAN"

22 May 2016   7:03 pm

Na Jesse Ngoty

Umri wa kuishi barani Afrika unaongezeka kwa haraka ikiwa ni maradufu sawa na maeneo mengine duniani kulingana na shirika la afya dunia WHO.

Rwanda ndiyo inayoongoza Afrika Mashariki, umri wa kuishi nchini humo ukiwa miaka 66.1.
Ripoti ya WHO inasema tangu mwaka 2000, umri wa kuishi umeongezeka kwa takriban miaka 10 zaidi. Kwa sasa mtu wa wastani anaweza kuishi hadi miaka 60.
Lakini Umri huo bado ni miaka 20 chini ya mtoto anayezaliwa katika mojawapo ya mataifa 29 yenye mapato makubwa.
Daktari Ties Boerma kutoka WHO ameimbia kipindi cha Newsday cha BBC kwamba sababu moja ni kupungua kwa vifo miongoni mwa watoto inayofanywa na chanjo.
Haya hapa mataifa yenye viwango vya juu vya umri wa kuishi Afrika:
  1. Algeria - 75.6
  2. Tunisia - 75.3
  3. Mauritius - 74.6
  4. Morocco - 74.3
  5. Cape Verde - 73.3
  6. Seychelles - 73.2
  7. Libya - 72.7
  8. Misri - 70.9
  9. Sao Tome - 67.5
  10. Senegal - 66.7


MugabeImmage c

Taifa la Ethiopia ni la 16 katika orodha hiyo likiwa na kiwango cha kuishi cha wastani wa miaka 64.8, Kenya ikiwa ya 22 na miaka 63.4,Ghana iko katika nafasi ya 25 ikiwa na miaka 62.4, Somalia ni ya 47 ikiwa na miaka 55 na Nigeria ni ya 48 ikiwa na miaka 54.5.

Umri wa kuishi katika eneo la Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara:

Algeria75.6
Mauritius74.6
Cabo Verde73.3
Ushelisheli73.2
Sao Tome na Principe67.5
Senegal66.7
Rwanda66.1
Gabon66
Namibia65.8
Botswana65.7
Madagascar65.5
Ethiopia64.8
Eritrea64.7
Congo64.7
Comoros63.5
Kenya63.4
Mauritania63.1
Afrika Kusini62.9
Ghana62.4
Uganda62.3
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania61.8
Zambia61.8
Niger61.8
Liberia61.4
Gambia61.1
Zimbabwe60.7
Benin60
Burkina Faso59.9
Togo59.9
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo59.8
Burundi59.6
Guinea59
Swaziland58.9
Guinea-Bissau58.9
Malawi58.3
Mali58.2
Equatorial Guinea58.2
Msumbiji57.6
Sudan Kusini57.3
Cameroon57.3
Nigeria54.5
Lesotho53.7
Côte d'Ivoire53.3
Chad53.1
Jamhuri ya Afrika ya Kati52.5
Angola52.4
Sierra Leone50

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.