PLUIJM : YANGA TUNAWEKA REKODI MPYA AFRIKA




16 May 2016

YANGA ndiyo mabingwa Tanzania unajua kocha wao Hans Pluijm amesemaje juu ya mafanikio yao? Ni hivi, ametamka kwamba baada ya rekodi hiyo sasa wanataka kufanya kitu tofauti katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Pluijm amesema kutokana na kufika katika hatua muhimu ya kutinga katika makundi ya mashindano hayo sasa anataka kufuta historia mbaya ya Yanga kwa kufika mbali katika kombe la shirikisho.
Raia huyo wa Uholanzi amesema kitu pekee kinachompa jeuri ya kuona hilo ni juu ya kikosi chake licha ya kufika mwisho mwa msimu lakini bado wachezaji wake wanaonesha kuwa tayari kwa mechi zaidi.
“Tunastahili kupata sifa na mafanikio ya namna hii, tumekuwa na msimu mgumu na bora ambao utulivu wetu na viwango vyetu vimetufanya sasa kutembea kifua mbele, tunaweza kupata mafanikio zaidi katika Afrika msimu huu,” amesema Pluijm.
“Angalia timu yangu, tuko mwisho mwa msimu lakini bado timu inaonekana kuhitaji kucheza zaidi, akili yetu sasa ni kuhakikisha tunafika mbali katika mashindano ya Afrika hii ni nafasi muhimu kwetu kuipa sura mpya klabu hii.”

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.