LOWASSA, MBOWE NA MNYIKA WAKAMATWA NA POLISI JIONI YA LEO



Viongozi wa Chadema wamekamatwa na polisi na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema; “Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kikao walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo lililokataza mikutano.”

Lowassa na viongozi wengine wakitoka katika kikao

Waliotakiwa kufika makao makuu ya polisi, ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe; mjumbe wa Kamati Kuu na waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa; Katibu Mkuu, Vicenti Mashinji na naibu katibu mkuu (Bara), John Mnyika.

Mkutano wa kamati kuu ya Chadema, umeitishwa ili kujadili ufanikishaji wa maandamano ya oparesheni UKUTA.

Mnyika na viongozi wengine wakiwa nje ya ukumbi waliofanyia kikao chao 


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.