NEWS UPDATES: POLISI WANAENDELEA NA MAPIGANO NA MAJAMBAZI MKURANGA,, YADAIWA MAJAMBAZI KADHAA YAMEUAWA
Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani asubuhi hii.
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yamefika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkurang, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru yamefungwa kutokana na mapambano hayo.
Majambazi ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa kuuwawa katika mapigano hayo kati yao na polisi huko Vikindu, wilaya ya Mkuranga leo.
Milio ya risasi na mabomu vilisikika kuanzia saa saba usiku katika eneo hilo ambalo majambazi hayo walikuwa wamejificha.
Habari zilizotufikia hivi punde, zinaeleza kuwa Polisi wameweka kizuizi cha barabara eneo la Kongowe, wilayani Mkuranga ambapo magari yote yanayotoka na kuingia Dar yanapekuliwa.
No comments:
Post a Comment