WANAVYUO WA CHUO CHA IFM WALALAMIKIA UONGOZI WA CHUO JUU YA TATIZO LA KUCHELEWESHEWA FEDHA ZA KUJIKIMU NA ZILE ZA FIELD

Image result for institute of financial management dar es salaam

Dondoo Vyuoni

Ikiwa tunafikia mwisho wa mwezi wa 8, katika upande huu wa Dondoo Vyuoni... leo nimekitupia jicho chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM ) 

Nilipata nafasi ya kuongea na baadhi ya wanachuo wa chuo cha IFM ambapo katika kujua maendeleo ya masomo na maisha ya chuoni hapo,  wanachuo hao wamelalamikia swala la kucheleweshewa fedha za kujikimu ambapo wameeleza kuwa ni tatizo ambalo linakua sugu sasa.

Wanavyuo hao wameongeza kuwa, mbali na kuchelewa kwa fedha za kujikimu katikaa mafunzo ya vitendo yaani field kuchelewa kutokana na sababu zilizo elezwa na Waziri wa elimu Mh. Ndalichako  fedha izo ambazo tayari zimepelekwa vyuoni wanachuo hao wanalalamikia kutokupewa hizo fedha kwa wakati wakati wamesha tia saini za kupokea fedha izo . 

Kufuatia malalamishi hayo,  kuchelewa kwa fedha izo kunapelekea wanafunzi hao kushindwa kufanya mafunzo hayo ya kujifunza kwa njia ya vitendo kwa ufanisi na wakati mwingine kushindwa kufika kabisa maeneo yao ya kujifunza kwani wanakosa nauli na fedha ya kula kwani wanategemea fedha izo. 

Aidha, wanachuo hao wameongeza kuwa hakuna mawasiliano/ mahusiano ya uhakika kati ya uongozi wa chuo na serikali ya wnafunzi chuoni hapo kwani wamekua wakiawaahidi fedha zitaingia lakini hawazipati katika ule muda tajwa. 

Jitihada za kuwapata viongozi wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo ili kuongelea swala hilo ziligonga mwamba kwani kwa sasa chuo kimefungwa na wanfunzi wako likizo lakini ntazidi kufuatilia na kukusogezea karibu yako mtu wangu...


" Kwa Dondoo mbalimbali zinazotokea katika vyuo vikuu vya Tanzania, kaa karibu yangu kupitia upande huu wa Dondoo Vyuoni ambapo ntakua nakusogezea karibu yako taarifa mbali mbali zinazoendlea vyuoni uko!! " 

   FACEBOOK, TWEETER, INSTAGRAM @ JESSENGOTY

                   >>>> USIKUBALI KUPITWA .. TEMBELEA 
                                                        
                                        WWW.JESSENGOTY.COM  

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.