IDRIS SULTAN APIGWA CHINI KUSHEREHESHA TUZO ZA MTV MAMA BONDENI MWEZI UJAO
Mchekeshaji wa Afrika Kusini anayefanyia kazi nchini Marekani, Trevor Noah, ametangazwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za mwaka huu za MTV MAMA.
Awali Idris Sultan, Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kevin Hart (Marekani) walikuwa miongoni mwa washereheshaji wengine waliokuwa wanafikiriwa.
Tuzo hizo zitafanyika October 22, 2016, kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini. Yemi Alade, Ycee, Cassper Nyovest na Alikiba wanatarajiwa kuwasha moto kwa kutumbuiza.
No comments:
Post a Comment