KAMPUNI YA ACCER YAZINDUA LAPTOP YA KWANZA YENYE KIOO CHA KUJIPINDA +PICHA
Kampuni ya Acer imezindua laptop ya kwanza ilio na kioo kilichojipinda.Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.
Televisheni kadhaa pia zimetumia uvumbuzi huo,lakini umezua mgawanyiko kwa kuwa una umuhimu na ubaya wake.
Kampuni hiyo ya Taiwan pia ilitangaza kwamba imefanikiwa kupata tekenolojia ya pet katika mkutano na wanahabari mjini Berlin.
Kampuni kadhaa za kielektroniki ikiwemo Samsung,Lenovo,DJI,Sony na Huawei zinatarajiwa kuzindua sura mpya ya laptopu zake katika maonyesho ya kiteknolojia ya Ifa katika mji mkuu wa Ujerumani wiki hii.
Laptop hiyo ina kioo kikubwa ikilinganishwa na laptop ya kawaida ya Acer,lakini ni umbo lake ambalo liliifanya kampuni hiyo kudai kuwa ya kwanza kuzinduliwa duniani.
No comments:
Post a Comment