KIONGOZI WA MILA :TUKIO LA KUPATWA NA JUA NI ISHARA YA MUNGU KUMKUBALI RAIS MAGUFULI, AELEZA STORY HII YA KALE

Image result for kupatwa kwa jua

Wakati wakazi wa Mbeya wakishuhudia tukio la kupatwa kwa jua muda huu unapoisoma habari hii, kati ya saa 4 hadi saa 6 tukio hilo linaatokea wakati mamia ya watalii wakifiika Tanzania kulishuhudia, hapo jana kiongozi mmoja wa mila alisema ni Ishara ya Mungu kumkubali Rais Magufuli. 

Katibu  huyo wa Mila wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, Mwanasimtwa Mwagongo, amesema tukio la kupatwa kwa jua linalotarajiwa kutokea Alhamisi hii katika Kijiji cha Rujewa wilaya ya Mbarali, ni ishara ya Mwenyezi Mungu kuukubali uongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania (TAJATI) nyumbani kwake katika Kata ya Isisi, Mwagongo alisema tukio hilo la kupatwa kwa jua nchini si mkosi, bali ni sawa na taa iliyokuwa imezimika na sasa imewashwa na kuongeza, hii ishara kuwa Mungu ameukubali utawala uliopo madarakani na ndiyo sababu ametoa giza na kuleta nuru.

Image result for kupatwa kwa jua

“Hapo zamani watoto walikuwa hawaruhusiwi kutoka nje siku ya tukio hili, Wazee waliamini ni ajali ya kugongana jua na mwezi na wanaoumia ni wanadamu hasa watoto kwa kusababishiwa milipuko ya magonjwa mbalimbali,” alisema.
“Lakini kwa sasa tunatambua kuwa ni tukio la kisayansi na kutokea kwenye eneo letu ni neema kutoka kwa Mungu. Kupitia tukio hili dunia itaijua Tanzania, itaijua Mbarali na itaijua Rujewa. Ni tukio ambalo limetutangaza”.
Aidha Mwagogo alisema baada ya tukio hilo, wazee wa kimila watachinja ng’ombe kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa neema ya tukio hilo na pia kumwomba aiepushe jamii na madhara yoyote yanayoweza kujitokeza.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.