MAMBO MAKUU YA KUZINGATIA KABLA NA BAADA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI

#friday XO

FRIDAY XO 

Kwa watu wanaotarajia kuanzisha mahusiano thabiti na yenye malengo pamoja na wale ambao tayari wamo ndani ya mahusiano ya aina hiyo, FRIDAY XO  imekuandalia vitu vya kuzingatia karibu tuyaone hayo yakuzingatia...

>>> Usidanganyike na muonekano wa nje au yale maongezi ya mwanzoKila mtu hua mstaarabu siku za mwanzo hata wale ambao sio.

>>> Usikimbilie kutangaza nia haraka, Siku zote ni rahisi mtu kua muwazi kwa rafiki yake kuliko kwa mtu ambae anajua anataka mahusiano nae kwa hofu ya kumpoteza.

" Tumieni muda wakutosha kufahamiana kama marafiki kabla hamjajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi."

>>> Uliza maswali kuhusu vitu ambavyo ni muhimu sana kwako.
Kwa mfano kama ni mtu wa familia au sio taka kujua mawazo yake kuhusu watoto hii itaepusha migongano isiyo ya lazima hapo baadae.

>>> Penda kujua malengo yake ya baadae, Hii itakuwezesha kugundua ni mtu wa aina gani kama ni mpenda maendeleo,mtu wa starehe tu n.k.

>>> Kuwa muwazi,:Hii inakwenda kwa pande zote kuna vitu ambavyo ukimwambia mtu ni vidogo sana ila ukificha vinakua kwa vile tu ulifanya siri.

>>> Hakikisha uwezo wenu wa kuelewa unaendana.
Hapa siongelei darasa ila mnavyokua sambamba kwenye maongezi ya kawaida tu yasiyo hitaji degree.

>>> Onyesha Misimamo yako hata kama unaona ni migumu kueleweka.
Ni vizuri mtu akikubali/taka kujiingiza kwenye mahusiano na wewe awe akijua atakua na mtu wa aina gani kama hupendi nguo fupi,mwanamke/mwanaume mnywaji wa pombe, mvuta sigara n.k sio unasubiri mpaka muwe pamoja ndo muanze kuzozana.
.
>>> Hakikisha kuna vitu Mnavyo Shabihiana
Ni muhimu mkiwa na vitu mnavyoweza kufanya pamoja iwe ni kuangalia movie ama kutembea nyakati za jioni inasaidia kuimarisha ukaribu wenu kuliko kila mtu kwenda na njia yake.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.