GAVANA WA MOMBASA BAADA YA KUMLETA CHRIS BROWN, ASEMA SASA NI DHAMU YA NICK MINAJ

Image result for NICKI MINAJ

Baada ya mwimbaji staa wa Marekani Chris Brown kufanya show weekend iliyopita Mombasa, Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye inaelezwa ndiye alidhamini tamasha la Mombasa Rocks Music Festival amedhaminia tena kumleta staa mwingine mwanadada Nick Minaj.

Gavana huyu inayedaiwa ana pesa za kutosha, ametangaza kuwa timu yake imeanza mazungumzo na uongozi wa rapper Nicki Minaj ili aje Mombasa kutumbuiza hivi karibuni.
Image result for GAVANA JOHO MOHAMED WA MOMBASA
GAVANA JOHO AKIWA NA RAIS UHURU KENYATTA
Jamal Gaddafi aliyekua MC kwenye tamasha la Mombasa Rocks  Music Festival amesema amepewa taarifa na Joho, awambie mashabiki wajiandae kwa show nyingine kubwa ya Nicki Minaj.
Inadaiwa sababu kubwa hasa ya Gavana huyo kuwaleta mastaa wakubwa kutoka Marekani ni kutaka kukuza jina lake na kuitangaza zaidi Mombasa kwenye suala la utalii.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.