" NATAMANI SIKU MOJA MALAIKA WAZIME MITANDAO " ASEMA JPM

Image result for MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amechukizwa na jinsi watu wanavyozusha mambo ya uongo katika mitandao ya kijamii.

Akiongea Jumatano hii wakati wa uzindizi wa ndege mpya mbili za ATCL aina ya Bombardier zilizonunuliwa kwa fedha taslimu za kodi za wananchi kutoka Canada, Rais Magufuli ameshangaa kuona watu katika mitandao ya kijamii wakiandika gharama za manunuzi ya ndege hizo wakati hawajui chochote.
Image result for MAGUFULI AKIZINDUA NDEGE ATCL
“Mtu mwingine anasema ndege hizo tumezinunua kila ndege dola milioni 61 wakati mimi najua ndege moja haikufika hata nusu ya hiyo bei, na anapost pale anaandika uongo, halafu hata akishajua ukweli wake baadaye wala hatubu."
Nilikuwa natamani siku moja malaika washuke waizime hii mitandao yote ili baada ya mwaka mzima itakapokuja kufunguka wakute sisi tumeshatengeza Tanzania yetu mpya, wanapost vitu vingine vya ovyo, wanasema no research no right to speak,” alisema Magufuli.
Pia katika uzinduzi huo, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuwafukuza kazi mara moja watendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania(ATCL) watakaokwamisha ufanisi wa huduma za kampuni hiyo.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.