MAGANDA YA MACHUNGWA YAMEMPA TUZO ZA MAONESHO YA GOOGLE

Maganda ya chungwa yamshindia tuzo la Google

Msichana wa miaka 16 nchini Afrika Kusini amejishindia zawadi ya maonyesho ya Google kwa kutumia maganda ya chungwa kutengeza kifaa kinachosaidia udongo kuhifadhi maji.
Kiara Nirghin aliwashinda wanafunzi wengine duniani kwa kujipatia ufadhili wa masomo wenye thamani ya dola 50,000 kwa ''kukabiliana na kiangazi kupitia chungwa''.
Kazi yake inajiri kufuatia kiangazi ambacho kinaendelea kuathiri Afrika Kusini.
Kiara Nirghin
Kiangazi hicho ambacho ni kibaya zaidi kuwahi kutokea tangu 1982 kimeathiri mimea huku mifugo ikifariki.
Kwa sasa anatumai kwamba mbinu hiyo inaweza kuwasaidia wakulima kuhifadhi fedha pamoja na mimea.

No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.