SERIKALI YA JPM KUWAPELEKA WATOTO WA MITAANI " JKT " WAKALITUMIKIE TAIFA LAO KWA UZALISHAJI MALI


Serikaly ya JPM inakusudia kuwapeleka katika kambi za mafunzo  ya Jeshi la Kuujenga Taifa (JKT) watoto wa mitaani wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ili wajifunze  stadi za kazi na shughuli  za uzalishaji mali.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  wakati wa mahojiano maalum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoandaliwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na Televisheni ya Taifa (TBC1).

Waziri Ummy alisema hatua hiyo inalenga kuliwezesha kundi hilo la vijana kujihusisha na shughuli za uzalishaji mali badala ya kuzurura hovyo mitaani sambamba na kujihusisha na tabia na vitendo  vinavyokiuka maadili katika jamii.

Alisema tayari  watendaji wa Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Waziri Mkuu tayari wamekutana kujadiliana kuhusu suala hilo ili kuangalia namna bora zaidi ya kusadia kundi hilo.

Alifafanua kuwa vituo vingi vya kulelea watoto hao vimekuwa na watoto waliozidi umri wa miaka 18, ambapo kwa mujibu wa sheria hawatakiwi kuwa katika vituo hivyo na kuongeza kuwa  ofisi yake itahakikisha zoezi la kuwapeleka katika mafunzo hayo linatekelezeka.


No comments:

This Website Is Developed & Maintained By Jesse. Powered by Blogger.