TAARIFA NZURI KWA MASHABIKI WA DAVIDO,SONY MUSIC KUACHIA KAZI ZAKE SOON!!
September 22, 2016 mtu wangu wa nguvu, nakusogezea taarifa nyingine nzuri kutoka kwa Davido star wa muziki kutoka nchini Nigeria ambaye alisaini deal na ya kufanya kazi na lebo ya Sony Music. Taarifa hii nzuri ikufikie shabiki wake uliyezimiss kazi za Davido kwenye Radio na TV.
Kimya cha takribani miezi kumi na moja cha msanii Davido huenda kikamalizika siku chache kutoka sasa, Hii ni baada ya star huyo anayesimamiwa kazi zake na lebel ya RCA records iliyoko chini ya Sony Music, kupost video akiwapa taarifa kuanza kuachiwa video zake zaidi ya 20 kabla mwaka 2016 haujaisha.
Davido kupitia video hiyo amesema anapanga kwa kuumaliza mwaka 2016 kwa style tofauti ili afanane na label yak, Sony Music ambao amedai kuwa wamemruhusu kuanza kuachia kazi zake ikiwemo albam yake mpya itakayoitwa Son of Mercy, ambayo itatoka ndani ya mwaka huu.
Davido alisaini deal ya usimamizi wa kazi zake na kamouni ya Sony Music, January 20 2016 ambapo Taifa la Nigeria lilikua taifa la kwanza barani Afrika kuingia makubaliano hayo na kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kutia saini ya record deal hiyo.
Mtazame Davido akiongelea hilo hapa chini.
No comments:
Post a Comment