TAJIRI WA KWANZA AFRIKA - DANGOTE KUINUNA KLABU YA MPIRA YA ARSENAL YA UINGEREZA
Dangote ambaye ni tajiri namba moja Afrika, ameiambia runinga ya Bloomberg mjini New York Jumatano hii kuwa anasubiri biashara zake kuimarika pamoja na uwekezaji wake wa ujenzi wa bomba la gesi na kiwanda cha kusafisha mafuta kabla ya kukinunua klabu hicho.
“Hakuna tatizo kwamba nitainunua klabu hiyo, na si tatizo la fedha,” alisema Dangote katika mahojiano na runinga ya Bloomberg.
“Pengine miaka mitatau au minne. Swala ni kwamba tunachangamoto nyingi. Ninahitajika kukabiliana nazo mwanzo baadaye nitaangazia swala la ununuzi huo,”
Dangote ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal amepoteza kiasi cha dola bilioni 4.4 mwaka huu kutokana na kushuka kwa thamani ya sarufi ya Nigeria.
Iwapo atainunua timu hiyo basi atakuwa mtu wa kwanza kutoka barani Afrika kumiliki timu iliopo katika ligi kuu ya Uingereza.
Bofya hapa kuona show hiyo kwenye bloomberg TV >>>Bloomberg
No comments:
Post a Comment